Latest Post

 
Ni muda mrefu sasa wanafunzi wa elimu ya juu wamekua wakilalamikia bodi ya mikopo hapa nchini,hatimaye kilio kimesikika na wamekuja na njia hii.
Bodi ya mikopo ya elimu ya juu nchini imesema kwasasa imekwishaimarisha mifumo yake ya kupokea na kushuhulikia malalamiko ya wanafunzi haswa kwa waliokosa mikopo kwenye bodi hiyo.
Hayo yamebainiswa na meneja wa habari, elimu na mawasiliano wa bodi hiyo Bwana Omega Ngole huku akisema bodi hiyo kwasasa imejipanga vyema katika kuhakikisha wanafunzi wanaomba mikopo wanapata mikopo kwa wakati. 
Bwana Omega Ngole ametoa wito kwa mafisa mikopo wa vyuo hapa nchini kuhakikisha wanabainisha matatizo ya wanavyuo na kuyashuhulikia kwa wakati ili kupunguza migogoro ya wanavyuo hao katika upatikanaji wa mikopo.
USIACHE KUCOMENT THEN LIKE ILI USHEE NA WANA

Hiyo picha unayoina hapo juu ni moja ya ukurasa kwenye mtandao maarufu nchini South Africa ambao ulipost ukiandika kuwa,Nanukuu"AKA AMEKUA MSANII WA KWANZA AFRIKA KUSINI KWA KUPATA WATAZAMAJI MILION MOJA KWA SIKU KUMI,VIDEO MPYA YA AKA MAKE ME SING ALIYOMSHIRIKISHA RAPA WA KENYA DIAMOND PLATNUMZ  IMEMFIKISHA MBALI MSANII HUYO WA AFRIKA KUSINI(AKA)
VIDEO YA MAKE ME SING IMEFIKISHA WATAZAMAJI MILION MOJA KWA SIKU KUMI TU NAKUMFANYA AKA KUWAMSANII WA KWANZA AFRIKA KUSINI KUFIKIA. "MWISHO WA KUNUKUU.
Nadhani unajua nini kitawasibu wakenya baada ya kujitangazia Diamond ni msanii wao,Hawa jamaa wanaonekana wezi sana maana walishawahi kusema Mlima Kilimanjaro ni wa kwao Saizi Tena Diamond wao,Toa neno moja tu kwa Wakeya na hawa wasauzi,Usiache kucoment hapo chini then shea na wana.


Ni Airlander 10 imegharimu miaka mitatu mpaka kukamilika kwake,ndege hiyo inaurefu sawa na uwanja wa mpira yaani mita 100,lakinipia inauwezo wa kubeba hadi tani 10 za mizigo,kwa mujibu wa  Kampuni inayotengeneza ndege hiyo wanadai kwamba Airlander ndio ndege bora zaidi kwakua haina kelele na tena inauwezo wa kushuka kama Helikopta tofauti na Aeroplane.
Airlander ina thamani ya dollar bilion 1 za kimarekani kwa ufupi ni jumla ya utajiri wa Mohamed Dewji (MO) na itafanyiwa majaribio mweziwa tatu mwaka huu.
Hii ni sehemu ya Engine

MAFUNDI KAZINI
USIACHE KUSHEA NA WANA

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Ernest Mangu amefanya Mabadiliko kwa baadhi ya Makamanda wa Polisi wa mikoa na vikosi hapa nchini.

Mabadiliko hayo ni pamoja na aliyekuwa kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro Kamishna Msaidizi Mwandamizi SACP Leonard Paul amehamishwa kwenda kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga na nafasi yake kuchukuliwa na Kamishna Msaidizi Mwandamizi SACP Ulrich Matei aliyekuwa Mkuu wa Utawala Kanda Maalumu ya Dar es Salaam.

Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Mihayo Msikhela aliyekuwa kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga amehamishwa kwenda kuwa Mkuu wa Kikosi cha Kuzuia dawa za kulevya.

Aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Ramadhani Mungi anaenda kuwa Kamanda wa Polisi Kikosi cha Bandari na nafasi yake inachukuliwa na Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Wilbrod Mtafungwa ambaye alikuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe.

Aliyekuwa Afisa mnadhimu Mkoa wa Iringa Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Prudenciana Protas anakwenda kuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Njombe.

Aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Philipo Kalangi amehamishiwa Makao Makuu ya Polisi na nafasi inachukuliwa na aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi mkoa wa Shinyanga ACP Ramadhan Ng’azi.

Aidha,Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Camilius Wambura anakwenda kuwa Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam na nafasi yake kuchukuliwa na Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Francis Massawe kutoka Makao Makuu ya Upelelezi Dar es Salaam. Aliyekuwa Afisa Mnadhimu Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Gilles Mroto anakwenda kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Tarime/Rorya kuchukua nafasi ya Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Gemini Mushi aliyehamishiwa Makao Makuu ya Upelelezi Dar es Salaam.

Wengine ni pamoja na Naibu Kamishna wa Polisi DCP Hezron Gimbi anayetoka Upelelezi Makao Makuu Dar es Salaam kwenda kuwa Mkuu wa Utawala Kanda Maalumu Dar es Salaam pamoja na aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Costantine Massawe anakwenda kuwa Mkuu wa Oparesheni wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam.

Mabadiliko hayo ni ya kawaida kwa mujibu wa Sheria, kanuni na taratibu za Jeshi la Polisi.
#USIACHE KUSHEA NA WANA

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.